MAJIBU YA AFANDE SELE KWA CHID BENZ
Baada ya juzi CHIDI BENZ kukubali kwamba pamoja na AFANDE SELLE kumdis, yeye bado yuko tayari kufanya nae kolabo ambayo alipanga kufanya na Afande wiki moja au mbili kabla hajamdis, Afande nae ametoa sentensi ya jibu kutokana na alichosema ChidiBeenz. Afande amesema “yeah mi niko tayari, niko pamoja nae Chidi anajua hilo, na hiyo kitu alishaniambia kitambo tukapanga na mimi bila shaka matatizo yaliyotokea ni mambo ya kupita lakini mimi wimbo wake hata kesho nasububiri beat niandike tufanye kitu kilichobora zaidi nafikiri itakua na maana kuliko malumbano malumbano yanayoendelea haya sio mazuri, sina beef nae” Chanzo cha beef yao ni baada ya Afande kuhojiwa East Africa Radio na kufananisha kuondoka kwa Ditto watu pori kwenda La Familia, sawa na kuondoka Manchester United na kwenda timu ndogo kama Bolton, maneno ambayo yalimkasirisha sana Chidi Benz