ALICHOKISEMA CHIDI BENZ KUHUSIANA NA AFANDE SELE
Pamoja
na kwamba watu wanaona ni beef imeanza kati ya Afande Selle na Chidi
Beenz, exclusive na millardayo.com rapper Chidi Beenz amesema wiki moja
kabla ya Afande Selle kumdiss on East Africa Radio, alikua amepanga
kumtafuta kwa ajili ya kumpa shavu la single yake mpya anayotaka
zisikike sauti za Mwana FA na Afande Selle.
Amesema “wiki moja kabla nilikua niko na Tippo wa Zizzou tulikua
tunaongelea ngoma flani hivi niliwahi kurekodi nikaanza kurekodi chorus
alafu nikaiacha, nikamtumia Mwana FA aandike verse yake pia ngoma
inaitwa Mani, Zizzou akaniambia ukimtumia na Afande itakua poa anaweza
kuandika kitu kizuri sana alafu hajasikika siku nyingi itakua safi,
nikasema kweli bwana hata mimi sijamsikia Afande zamani itabidi nikifika
Dar nimtafute kwenye simu”
Mfalme wa Ilala amesema “yani juzi nimesikia Afande ananidiss nikacheka,
nikaona Afande juzi tu tumekutana kwenye show ya CLOUDS nimemuona
Afande anazurura peke yake nikamuita nikiwa na Fid Q, Prof J, FA na
wengine nikamwambia Afande njoo tupige picha mpaka leo ninayo, watu
walicheka wakafurahi pia, sasa from no where Afande amenidiss mimi
wakati mi sijawahi kusema chochote kibaya kuhusu yeye”
Kwa kumalizia CHIDI amesema “sijaufuta huo mpango wa kufanya kolabo na
Afande Selle, namfahamu ni mtu mmoja anabadilika kwa haraka sana na
kuomba sana msamaha, wazo la kufanya nae kolabo bado ninalo na kama
atakubali tutarekodi, hakuna sababu ya kugombana wala kusemana”
Chanzo cha haya yote ni wakati Afande Selle alipofananisha kitendo cha
mwimbaji DITTO kuondoka kwenye kundi lake la WATU PORI na kwenda LA
FAMILIA ya CHIDI BENZ, sawa na kuondoka MANCHESTER UNITED kwenda
WOLVERMPTON.
Akiamplfy na millardayo.com march 26 2012, Chidi alikanusha taarifa
kwamba atamteka na kumpiga Afande Selle vilevile akamuonya JAY MOE
kutoingilia chochote kati yake na Afande Selle huku akisisitiza kwamba
“hata nilivyomuona na Jay Moe kwenye ile interview namuona Jay Moe, Jay
Moe ni nini bwana vitu anaongea Jay Moe pale na Afande wote kabila moja,
ni watu ongea sawa”
Chidi amesema hatofanya chochote kama ikitokea akakutana na Afande Selle
sehemu yoyote
Comments
Post a Comment