STEVEN KANUMBA AFARIKI DUNIA
Habari
zilizotufikia hivi sasa zinasema msanii maarufu nchini, Steven Kanumba
amefariki dunia ghafla baada ya kudondoka na kujingonga sehemu ya kisogo
akiwa nyumbani kwake Vatican, Sinza jijini Dar es Salaam. Tukio hilo
limetokea majira ya saa 7 usiku wa kuamkia leo na taarifa za kudondoka
kwa Kanumba zilitolewa na kijana anayeishi nae hapo nyumbani ajulikanaye
kwa jina la Seti aliyemwita daktari kujaribu kuokoa maisha yake lakini
alipofikishwa hospitali ya Muhimbili tayari alikuwa amekata roho. Kwa
sasa mwili wa marehemu umeifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti
hospitali ya Taifa Muhimbili. Habari zaidi zitawajia baadae.
Comments
Post a Comment