ALICHOKISEMA DIAMOND BAADA YA WEMA KUMTUPIA KOMBORA NDANI YA XXL YA CLOUD FM
Baada ya
kukasirishwa na alichokisema Wema, Diamond aliomba kuzungumza kwenye
AMPLIFAYA ya CLOUDS FM na kukiri kwamba “Millard kiukweli mimi sipendi
ugomvi, na haya nisinge yasema kama yeye asingekuja kuongea uongo, yani
hata sababu kubwa ya mimi na yeye kutofautiana ilikua ni kitu kidogo tu
anakipeleka kwenye media na ikafika time anasema hanitaki ila mimi ndio
namng’anga’nia wakati ukweli ni kwamba alikua analetwa nyumbani na
rafiki zake na ndugu zake akilia anaomba isuluishwe turudiane, mpaka
anampigia mama yangu mzazi, rafiki zangu na ndugu kama Shetta na Romy
Jones, pia anawaambia marafiki zake waandae sehemu ya Dinner ili atokee
kama Suprise”
Diamond amesema
“kabla ya show yangu ya juzi alikuja nyumbani mimi niko ndani navaa
nasikia sauti yake barazani, namuuliza ndugu yangu Rommy ananiambia ni
Wema, nauliza kafata nini nyumbani? mimi nina mpenzi wangu na yeye
anamfahamu na hizi drama za Wema zinafanya mpenzi wangu akasirike kwa
sababu anaona bado naendelea na Wema, sasa pale nyumbani nilitoka nje
baada ya kukasirika ila wakanishika nisimguse, ndio wakamwambia aondoke…
yani baada ya kugundua kwamba mimi sitaki kuwa na yeye tena sasa
anatumia kama ile hautaki kuwa na mimi, Nakuharibia sasa”
“Wakati anakuja
kunipa hela kwenye stage mi nilikua naogopa kwa sababu tayari alikuja
nyumbani kabla yake ndio maana nilihisi anataka kufanya drama nyingine
tena ndio maana nikamkwepa na kujifanya kama sijamuona lakini akaganda
makusudi kama anataka kufanya kitu flani, mpaka mwisho baadae akamfata Q
Chief anamlilia pia kawafata mama yangu na mama mdogo anawaambia mimi
mtoto wenu nampenda sana ananitesa, alafu baada ya hapo anakuja kwenye
Media na kuongea vitu vingine, na kunitengenezea mazingira ili mimi
nionekane mbaya” – Diamond
Katika sentensi
nyingine Diamond amethibitisha kwamba kwenye hiyo show yake kulikua na
wasichana wawili ambao waliwahi kuwa wapenzi wake, na walijitokeza pale
kwenye stage na kumpa pesa na yeye alizipokea bila tatizo kwa sababu
hana tatizo nao akiwemo Sarah ambae nlimwimbia “Nenda kamwambie” ila za
Wema alizikataa makusudi kwa sababu alikua anataka kutengeneza drama
manake ishu isingeishia pale.
Platnums
ameizungumzia ishu nyingine kwamba “hata nilipokua kwenye uhusiano na
yeye nilishawahi kumuonya Wema mara nyingi, niliku sipendi kuwa na mtu
anaeandikwa andikwa sana kwenye magazeti, kabla nilijua ni umaarufu
lakini nikagundua kwamba alikua anazipeleka stori mwenyewe tena na hela
ya kuwalipa waandishi anatoa, na kuna kipindi nililipa hela waandishi
wasiandike hizo habari lakini Wema akatoa zaidi ya hiyo, alikua
anapeleka stori mwenyewe, kama juzi alisikia naumwa niko hospitali
akanipigia kunipa pole…. kesho yake nikaona stori kwenye gazeti wakati
hakuna aliefahamu zaidi yake na stori imetoka vilevile, nikakasirika
sana”
“katika tukio
lililoniudhi zaidi ni pale nilipogundua alipopeleka stori ya kuniharibia
kwenye gazeti kwamba nina nuski na ishu nyingine kibao, baada
nikakutana nae nikamuuliza kwanini unapeleka hizo habari kwenye gazeti?
akazuga kwa kumpigia simu mwandishi na kuanza kumtukana mbele yangu
kwamba hizo habari ameandika tofauti, sio kama alivyomuhoji, lakini
baadae wakati nimeondoka alimpigia simu na kucheka huku akimwambia
tumemuweza leo, Wallah nimlale mama yangu mzazi hicho kitu ndio
kiliniuma nikaona bora tuachane kwa sababu niligundua ananitumia mimi
kufanya mambo yake, amesema yeye ndio alianza kuwa staa kabla yangu…..
ni sawa ila mimi kuanza kwangu nimekuja na akili, yeye anataka kutumia
wanaume mastaa apate umaarufu”
“Kilichonifanya
nijue kwamba amenizunguka kwenye ile habari ni wakati nilipokutana na
huyo mwandishi ambae alinithibitishia kwamba Wema mwenyewe ndio
aliipeleka ile habari na kweli baada ya kunizuga kwa kumtukana,
alimpigia simu mwandishi na kucheka baada ya mimi kuondoka” – Diamond
“Niliamua kuwa
kwenye mapenzi na Wema na kujipa moyo kwamba nitairekebisha tabia yake,
na nilikua napigiwa simu na watu mbele yake wakiniambia ananiharibia
nyota mpaka analia yani, nikawa namsafisha kwa watu kwamba hayuko hivyo
mpaka watu wakaanza kupenda uhusiano wetu, kumbuka baada ya yeye
kuachana na Kanumba alikimbia kwenda Marekani, akarudi tena bongo na
kuanza kunitongoza kwenye facebook kwa sababu alikua anajiuliza ataanza
kutoka na nani ili azidi kupata umaarufu” – Diamond
Leo kwenye
AMPLIFAYA ya CLOUDS FM Diamond ataendelea kufunguka Exclusive mambo
mengine hakutaka kuyasema kwenye Media lakini imebidi kwa sababu Wema
ameshindwa kujiheshimu na kutaka yeye aonekane mbaya, atataja pia moja
kati ya tukio la ajabu alilowahi kulishuhudia kwa Wema lakini hakulisema
wala halikuharibu chochote kwenye uhusiano wao, Diamond atafunguka pia
kuhusu rekodi ya Mauzo aliyoivunja kwenye show ya Mlimani City.
(AMPLIFAYA ni saa 1 usiku mpaka saa 3)
Comments
Post a Comment